0
CHELSEA imelazimishwa sare ya nyumbani ya kufungana bao 1-1 na Schalke ya Ujerumani katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya
makundi, Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London.

Kiungo Cesc Fabregas alitangulia kuifungia The Blues dakika ya 11 ingawa pia alionekana kuchezewa faulo kabla ya
kufunga. Klaas Jan Huntelaar aliisawazishia Schalke
dakika ya 60 na kumfanya kocha Mreno, Jose Mourinho aondoke ameinamisha kichwa uwanjani.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Courtois,
Ivanovic, Cahill, Terry, Filipe Luis, Matic,
Fabregas, Ramires/Oscar dk69, Willian/Remy dk74, Hazard na Drogba/Costa dk74.

Schalke: Fährmann, Höger, Ayhan,
Neustädter, Fuchs, Boateng, Aogo, Sam,
Meyer/Choupo-Moting dk74, Draxler na
Huntelaar.

Chapisha Maoni

 
Top