0
BAO pekee la Jerome Boateng dakika ya 89, limeipa ushindi mwembamba wa nyumbani, Bayern Munich wa 1-0 katika mchezo wake wa kwanza makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.

Man City ilizuia vizuri mashambulizi ya
Bayern kwa dakika 89 Uwanja wa Allianz
Arena kabla ya kuachia dakika za
mwishoni. Kocha Pep Guardiola aliyekuwa mnyonge muda wote wa mchezo, alitimka kwa kasi kutoka kwenye benchi kumfuata
Boateng kushangilia naye bao hilo.

Kikosi cha Bayern kilikuwa: Neuer, Rafinha/ Pizarro dk84, Boateng, Benatia/Dante dk84, Bernat, Alaba, Lahm, Alonso, Muller/Robben dk76, Gotze na Lewandowski

Man City: Hart, Sagna, Demichelis, Kompany, Clichy, Fernandinho, Yaya Toure, Navas, Silva, Nasri (Milner 58), Dzeko/Aguero dk74.

Chapisha Maoni

 
Top