Arusha, kumruhusu kutohudhuria siku za kesi na abaki magereza, kutokana na maumivu makali anayodai anayapata sehemu za siri alikominywa
na polisi na kuingiziwa mti kwenye haja kubwa.
“Mheshimiwa Hakimu naomba mahakama yako inipe ruhusa ya kutohudhuria siku ya kesi, sababu
ninapopanda gari napata maumivu makali sana sehemu za siri kunauma kwa sababu polisi walinitesa kwa kuniingizia mti kwenye haja kubwa
na kuminya sehemu zangu za siri,” alisema.
Alisema mbele ya Wakili wa Serikali, Rose Sulle kuwa mbali na maumivu ya sehemu za siri, pia mguu wake uliokatwa hospitalini, bado unamsumbua kutokana na maumivu.
Maginga pia aliomba iagize Magereza wamruhusu akatibiwe hospitalini, kwani alitakiwa kwenda kupata matibabu Septemba 5 mwaka huu, ila
alizuiwa hadi sasa. Akijibu hoja hizo, Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo,
Devotha Msofe, alisema suala la kuja
mahakamani ni lazima na mahakama haiwezi kumpa ruhusa hiyo.
Pia, alimshauri mshitakiwa huyo kuwa kama ana maelezo mengi, amweleze hakimu anayesikiliza kesi yake, Mustapher Siyani ambaye kwa siku
hiyo hakuwepo.
“Sikiliza Maginga suala la kuja mahakamani ni lazima na sio hiyari wala majadiliano, ila kuhusu
kwenda hospitalini liwasilishe Magereza ndio mtaona kwa pamoja mnafanyaje,” alisema.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa
washitakiwa hao wameshitakiwa kwa makosa yaliyo chini ya Sheria ya Kuzuia ugaidi, ambapo Sheria Namba 22 ya Mwaka 2002 inasema
upelelezi ukishakamilika, Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza na kutoa uamuzi.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kuua, kujaribu kuua, kusajili na kusafirisha vijana
kujiunga na Al-Shabaab.
Mbali na mashitaka hayo, pia wanahusishwa na
tukio la mlipuko wa bomu lilitokea baa ya Arusha Night Park jijini Arusha na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 16.
Watuhumiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ni Abdallah Athumani, Abdallah Thabiti, Ally Hamisi, Abdallah Wambura, Rajab Hemedi, Hassan
Saidi, Ally Hamisi, Yassin Sanga, Shaaban Wawa, Swaleh Hamisi, Abdallah Yassin, Abdallah
Maginga na Sudi Nassib Lusuma.
Wengine walioongezwa katika shauri hilo ni Shaaban Mussa, Athuman Hussein, Mohammed Nuru, Jafari Lema, Abdul Mohammed na Said
Michael Temba.
Chapisha Maoni