![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiA3aXHkmFb6UeGaNeCqV1kM6hBtm5t8Gohmuuq7Cr2xPhLFvszWYqChIFb-UZ7CfvDp68YX9b-lg6cC7kbaTMlm9IH-Q2Rb5ci_tC9LK-TgCpX_gg0Ft6a7lMNd4NfGGQr3Z2ECXu3wqsu/s350/1421162494835.jpeg)
ndani ya CCM zimeingia katika hatua
mpya baada ya mwanasiasa mkongwe,
Kingunge Ngombale - Mwiru kuibuka na
kudai kuwa wote waliojitokeza kuwania
nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa
wanatumia fedha kutaka kuingia Ikulu.
Kauli ya mwanasiasa huyo ambayo
imekuja siku moja kabla ya Kamati Kuu
ya CCM kukutana leo mjini Unguja na
moja ya ajenda ikitajwa kuwa suala la
maadili, inaweza kuwa mwiba mchungu
kwa wanasiasa hao ambao wanaongezeka kila kukicha.
Akizungumza Dar es Salaam jana,
Kingunge alisema: “Kuna suala la kukosa
uadilifu, kuna suala la matumizi ya pesa
na nikwambie ukweli, hao wanaotangaza
urais wote wanatumia pesa, wanatumia
faulo mbalimbali na wananchi wanajua.”
Kwa miezi kadhaa sasa, baadhi ya
makada wa CCM wamekuwa wakitajwa
kufanya harakati kichinichini na wengine
kushiriki shughuli za wazi zinazoashiria
kuwa wanataka kuwania nafasi hiyo ya
juu. Hadi sasa makada wanne tayari
wameweka wazi nia yao hiyo.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe na Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba kwa nyakati tofauti walitoa kauli zinazowashutumu makada wengine wa chama hicho kwa matumizi makubwa ya fedha katika kushawishi uungwaji mkono.
Hata hivyo, kauli za wanasiasa hao
zimedaiwa kuwa ni fitina za kisiasa kwa
kuwa wagombea wote wanatoa fedha,
bali wanazidiana viwango tu.
Mbali na Makamba na Membe, wanaCCM wengine waliotangaza au kutajwa kuwania urais ni Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Wengine ni mawaziri wakuu wa zamani,
Edward Lowassa na Frederick Sumaye,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano
na Uratibu), Stephen Wasira na aliyewahi
kuwa Waziri wa Nishati na Madini,
William Ngeleja.
Kauli ya Kingunge aliyoitoa kupitia
Televisheni ya ITV, imekuja wakati
wanasiasa sita miongoni mwa hao
wanaotajwa wakikaribia kumaliza miezi
12 ya uangalizi kutokana na onyo kali
dhidi yao lililotolewa na Kamati Kuu ya
CCM Februari 18, mwaka jana baada ya
kuwatia hatiani kwa makosa ya “kuanza
kampeni mapema na kufanya mambo
ambayo ni kinyume na maadili ya chama
na ya jamii.”
Wanaotumikia adhabu hiyo ni Lowassa,
Sumaye, Njeleja, Makamba, Wasira na
Membe.
Akisisitiza hoja yake hiyo bila kutaja
majina, Kingunge alisema makada hao
wamekuwa wakitumia fedha nyingi
kujitangaza na kutengeneza ushawishi
wa kukubalika kwa wananchi jambo
ambalo ni kinyume na maadili ya
uongozi.
Kingunge alisema mwanasiasa yeyote
anayehitaji uongozi hapaswi kutumia
fedha kushawishi wananchi wamchague.
“Kiukweli tukiangalia wote
wanaojitangaza hakuna msafi hata
mmoja... hatuwezi kuchagua rais kama
vile tunachagua wachezaji wa mpira,
haiwezekani. Tunataka kupata mgombea
wa urais ambaye atakuwa na uwezo wa
kushughulikia kwa vitendo kero na
umaskini wa Watanzania,” alisema
Kingunge.
Alisema badala ya viongozi kutumia
muda mrefu kumtafuta mchawi, ni
vyema wakatazama namna ya
kushughulikia suala la maadili kwa
sababu kati yao hakuna msafi hata
mmoja.
Kuhusu watu wengi kujitokeza kutaka
urais, Kingunge alisema: “Kujitokeza
kugombea urais siyo dhambi, ingawa
watu wanashangaa kidogo kwamba kila
mtu anaibuka tu anataka urais, kidogo
inaleta kasoro lakini siyo kitu, wanataka
kutumia haki zao.”
Mkongwe huyo wa siasa alisema
wananchi ndiyo wanaowajua wagombea
hao na sifa zao, hivyo wakumbuke kuwa
anayechaguliwa ni rais na siyo mchezaji
wa mpira.
“Mnachagua rais ambaye ataweza
kuwaunganisha kama Taifa, ataweza
kuwatumikia kwa vitendo siyo
kujitumikia wenyewe, pia ataweza
kutatua matatizo yanayowakabili
wananchi,” alisema.
Aliongeza kwamba kwa kuwa tatizo
kubwa la wananchi ni umaskini,
wananchi watazame mtu atakayeweza
kuondoa hali hiyo.
Akizungumzia kuhusu namna viongozi
wa Afrika wanavyoyatumia madaraka
yao, Kingunge alisema wamepiga hatua
kubwa lakini bado haitoshi kwa kuwa
wanakosa namna chanya ya kutumia
madaraka ambayo Afrika iliyapigania
kutoka kwa wakoloni.
“Tumeupigania uhuru ili tuendeshe nchi
yetu wenyewe, turudishe ile thamani
yetu kama watu. Sasa madaraka
tumepata, lakini tunayatumiaje?” alihoji.
Kuhusu Mapinduzi
Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyotimiza miaka 51 jana, Kingunge
alisema yamekuwa na faida kubwa kwa
Wazanzibari.
Alisema Mapinduzi hayo ndiyo msingi
wa Muungano ambao umeleta mafanikio
makubwa kwa pande zote licha ya
changamoto zinazoibuliwa.
“Haikuwa na budi kufanya mapinduzi
kwa kuunda kamati ya wapiganaji 14
ambao waliongoza kazi hiyo baada ya
kuona mfumo uliokuwa unatumiwa na
Serikali ya Sultan unawakandamiza
wazawa. Baada ya mapinduzi hayo
kufanikiwa, ardhi iliyokuwa inamilikiwa
na kundi moja la Waarabu ikagawanywa
kwa kila Mzanzibari akapata ekari tatu,
pamoja na hali hiyo elimu ilitangazwa
kutolewa bure.”
Africa Newss
Mwananchi
Chapisha Maoni