Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe,amelipongeza Kanisa la Anglikana
Tanzania kwa kusimama kidete kupinga
ndoa za jinsia moja, hata pale makanisa
mengine ya Anglikana duniani yalipounga mkono suala hilo.
Akizindua sherehe za Miaka Hamsini tangu kuanzishwa kwa Dayosisi ya Dar es Salaam ya Kanisa hilo jana, Mhe. Membe alisema msimamo huo wa Kanisa na Watanzania
uliipa serikali nguvu kukataa shinikizom
kutoka nchi za Magharibi kwamba
iidhinishe ushoga hapa nchini.
"Mlinitia nguvu sana pale niliposimama
kidete kuwaambia rafiki zetu wa nje kuwa katika hilo la ndoa za jinsia moja,
Tanzania tunaomba tukubaliane
kutokukubaliana," alisema Mhe. Waziri,
wakati wa uzinduzi huo uliofanyikia
kwenye kanisa la Mtakatifu Albano, jijini
Dar es Salaam. Sherehe za Miaka 50 ya
Dayosisi ya Dar es Salaam zitafikia kilele
Julai, mwaka huu.
Mhe. Membe alisema serikali itaendelea
kushirikiana na Kanisa la Anglikana na
madhehebu mengine ya dini kuboresha
maisha ya Watanzania.
"Naomba muendelee kushirikiana na
serikali katika kutoa huduma kwa
wananchi," aliwaambia waumini na
waalikwa wengine waliohudhuria misa
maalum ya uzinduzi iliyoongozwa na
Askofu Valentine Mokiwa.
Aliwataka viongozi wa dini kuombea nchi umoja na amani, na kuhimiza waumini wao kushiriki kikamilifu katika matukio mawili muhimu yanayolikabili taifa mwaka huu -- Kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Uchaguzi wa Rais ni muhimu kwa sababu "Rais wa Awamu ya Tano atategemewa kuendeleza mema ya Awamu ya Nne na awamu zilizopita, na kutoa majawabu kwa changamoto za sasa na zijazo na kutusogeza karibu zaidi na Tanzania njema tunayoitamani, Tanzania yenye neema tele.
Hatuko mbali na nchi yetu hiyo ya ahadi," alisema. Mhe. Membe alishambulia rushwa na
Ufisadi kuwa ndivyo vinavyodidimiza nchi na kuongeza umasikini kwa wananchi licha ya Tanzania kuwa na rasilimali lukuki.
"Tuchague viongozi waadilifu, wazalendo, wachapa kazi, wasio na uchu wa madaraka kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi na marafiki zao," alisema.
Alitaka vijana waandaliwe vyema kushiriki ujenzi na ulinzi wa taifa kwani ndio warithi. "Tukiwaandaa vyema,mustakabali wa taifa letu na watu wake utakuwa kwenye mikono salama. Tukishindwa leo, tutalia na kusaga meno kesho," alionya.
Waziri Membe akikaribishwa na AskofuMokiwa kwaajili ya utoaji wa vitabu vya
kuchangishia fedha kwa ajili ya miradi ya Dayosisi
Chapisha Maoni