Mashariki na Kati Azam FC, umetangaza
rasmi kuwatema wachezaji sita kwa
awamu ya kwanza huku nyota wawili
wakifeli majaribio.
Nyota hao walioachwa ni makipa Ivo
Mapunda, Khalid Mahadhi aliyekuwa
ametolewa kwa mkopo Mafunzo ya
Zanzibar, mabeki Said Morad, Racine Diouf
kutoka Senegal pamoja na washambuliaji
Didier Kavumbagu (Burundi) na Allan
Wanga (Kenya).
Akizungumza na mtandao rasmi wa
klabuwww.azamfc.co.tz Ofisa Habari wa
Azam FC, Jaffar Idd, alisema wachezaji hao
wameachwa wakiwa wamepata stahiki zao
kwa wale ambao waliokuwa wamebakiwa
na mikataba.
Alisema mbali na wachezaji hao, pia
wachezaji wawili kati ya wanne waliokuwa
kwenye majaribio nao wameachwa rasmi
ambao ni beki wa kushoto kutoka Ghana,
Nurudeen Yusif aliyetokea Medeama ya
huko na kiungo mshambuliaji David
Wirikom (Cameroon).
Wawili hao wamepewa majibu ya kufeli
majaribio yao leo asubuhi kufuatia Kocha
Mkuu Zeben Hernandez, kutoridhishwa na
uwezo wao kwa siku nne walizofanya
mazoezi na kikosi cha Azam FC.
“Wakati tunajiandaa na msimu mpya kuna
wachezaji tuliwaalika kutoka nchi
mbalimbali Afrika kwa ajili ya kufanya
majaribio, ambao mpaka sasa wapo wanne,
tangu tulipoanza mazoezi kwa siku
takribani nne mwalimu leo ameamua
kuwapunguza wawili na wawili wamebakia.
“Waliofeli majaribio ni David Wirikom
kutoka Cameroon na Nurudeen Yusif
kutoka Ghana, kocha ameona viwango
vyao havitofautiani sana na viwango vya
wachezaji wetu hapa nyumbani, kocha
ameongea nao leo mara baada ya mazoezi
na kuwaambia haoni kama wanaweza
kumsaidia kwa sababu anataka kuona mtu
wa kimataifa anayekuja awe zaidi ya
wachezaji wetu,” alisema.
Wachezaji wanaoendelea kwenye majaribio
ni makipa Daniel Yeboah (Ivory Coast) na
Juan Jesus Gonzalez (Hispania), ambao
wanawania nafasi moja ya usajili katika
eneo la golikipa.
Jaffar alimalizia kwa kusema kuwa
wanatarajia kuwapokea wachezaji wengine
wa kimataifa ndani ya siku mbili au tatu
zijazo kwa ajili ya majaribio yote ni katika
kuendelea
Chapisha Maoni