0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),
limeipiga faini ya dola 5,000 Klabu ya
Young African kwa kosa la kuchelewesha
mchezo baada ya wachezaji wake
kumzonga mwamuzi wakati mchezo wa
kuwania kuingia hatua ya makundi ya
Kombe la Shirikisho dhidi ya GD Sagrada
Esperanca uliofanyika Angola Mei 18,
2016.
Uamuzi wa mchezo huo Na. 100 ulifanywa
na Kamati ya Nidhamu ya CAF inayoundwa
Mwenyekiti Raymond Hack – Raia wa
Afrika Kusini na wajumbe Mustapha
Samugabo (Burundi) na Gbenga Elegbeleye
(Nigeria). Pia alikuwako Amina Kassem
kutoka Sekretarieti ya CAF ambaye ni
Mtawala katika Kitengo cha Nidhamu.
Katika mkutano huo uliofanyika Cairo,
Misri – Makao Mkuu ya CAF, Julai 3, 2016,
kamati ilipitia taarifa zote za mchezo na
kufikia uamuzi wa kuipiga faini Young
Africans.
Taarifa za mchezo zinasema, wachezaji wa
Young Africans walionyesha utovu wa
nidhamu kwa kumzonga mwamuzi na
kumsukuma mara baada ya kutoa adhabu
ya penalti kwa wapinzani. Kwa tukio hilo,
mchezo huo ulisimama kwa dakika sita.
Polisi waliingia uwanjani kudhibiti hali
hiyo.
Kwa kosa hilo, Wachezaji wa Young
Africans walivunja Ibara ya 82
inayozungumza utaratibu wa mawasiliano.
Kwamba chama chochote cha mpira wa
miguu, klabu, ofisa au mtu yoyote
wakiwamo wachezaji, lazima waheshimu
utaratibu za kuvumilia, uadiliufu na
uanamichezo.
Kwa mujibu wa Kamati hiyo ya Nidhamu
ya CAF, Young Africans ilistahili kutozwa
faini ya dola 10.000 za Marekani kwa
makosa ambayo si uungwana kwenye soka
yaliyoonyeshwa na wachezaji wake.
Lakini kwa kuwa Young Africans
haikuonyesha utovu wa nidhamu katika
mchezo mingine ya kimataifa iliyofuata
dhidi ya MOB ya Algeria na TP Mazembe
ya DRC, imepunguziwa adhabu na sasa
wametakiwa kulipa dola 5,000 za Marekani
kama faini. Faini hiyo haina budi kulipwa
mara moja. Na imetakiwa kuendelea kuwa
na nidhamu, vinginevyo adhabu hiyo
itawarudia.
Tayari Young Africans imepewa namba za
akaunti ya CAF inakotakiwa kulipa, lakini
pia imepewa fursa ya kukata rufaa kama
wataona kuna haja ya kufanya hivyo. Muda
wa kukata rufaa ni siku tatu baada ya
kupewa taarifa hiyo kwa maandishi.

Chapisha Maoni

 
Top