0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kimepanga kulisaidia Jeshi la Polisi
kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilitoa zuio la
mikutano ya siasa ya wazi na ya ndani nchini
kote, hata hivyo CCM imepanga kufanya
Mkutano Mkuu tarehe 23 Julai mwaka huu
mjini Dodoma.
Kwenye mkutano huo, Dk. Jakaya Kikwete,
Mwenyekiti wa CCM atakabidhi mamlaka hayo
kwa Dk. John Magufuli ikiwa ni utaratibu wa
kawaida wa chama hicho.
Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha)
limepanga kuzuia mkutano huo kwa madai ya
kulisaidia Jeshi la Polisi kusimamia agizo lake
kwa vyama vya siasa nchini.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana
jijini Dar es Slaam viongozi wa Bavicha
walisema, hatua hiyo ni katika kuhakikisha
wanalisaidia jeshi kutekeleza amri iliyotolewa
na Rais Magufuli ya kuzuia mikutano ya
vyama vya siasa hadi mwaka 2020.
“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka
mikoa yote nchini watakaokwenda Dodoma
kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya
mkutano usio halali wa CCM. Kwa sababau
Jeshi la Polisi limezuia mikutano yote ya siasa
kwa sasa.
“Pia ni katika kuunga mkono kauli ya Rais
Magufuli kwamba, hakuna mikutano ya vyama
vya siasa mpaka mwaka 2020. Huu ndio
msiamamo wa baraza.
“Mikutano yetu sisi kama Chadema tunazuiwa
lakini CCM wanafanya. Mahafari ya chama cha
mapinduzi yanafanyika. Ni jana CHASO
(Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
Chadema) Morogoro tumezuiwa lakini UVCCM
(Umoja wa Vijana wa CCM) Mkoa wa
Morogogo wamefanya na picha zipo. Hii sio
haki, kama mbwai na iwe mbwai,” alisema
Patrick ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa
baraza hilo.
George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa
Mbeya alisema “… ni kwamba, huko mikoani
vijana wameshajipanga. Wana ari kubwa ya
kwenda Dodoma.
“Tumeamua kufikia hatua hii kwa sababu
tumekuwa tunaona hakuna haki katika nchi
hii. Kuna mahafali yanafanyika vyuo vikuu,
wenzetu CCM wanaruhusiwa sisi Chadema
tunakatazwa.Vijana wa Chadema wamekuwa
wakikamatwa bila sababu za msingi,” alisema
Tito.

Chapisha Maoni

 
Top