0
Meneja mpya wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anapanga kutosafiri na mshambuliaji
mpya wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic Uchina.
Mourinho hata hivyo amepanga kuwachukua wachezaji wa England Wayne Rooney, Chris
Smalling na Marcus Rashford.
Klabu hiyo inapanga kucheza mechi mbili za
kujiandaa kwa msimu ujao na inapangiwa kuwasili
Uchina Jumanne.
Mourinho amesema Rooney, Smalling na Rashford hata hivyo hawatacheza dhidi ya Borussia
Dortmund mjini Shanghai tarehe 22 Julai na Manchester City mjini Beijing mnamo 25 Julai. Ibrahimovic, 34, huenda asishirikishwe hata
kidogo.
Akikosa kusafiri na timu hiyo bara Asia, basi mashabiki watasubiri muda zaidi kumtazama Ibrahimovic akicheza mechi yake ya kwanza United.
United wanatarajiwa kucheza dhidi ya Salford City
uwanjani Moor Lane mnamo 26 Julai.
Mechi hiyo ilipothibitishwa, Gary Neville, mmiliki mwenza wa Salford aliandika kwenye Twitter:
"Mechi ya kwanza kwa Zlatan!!"
United baadaye watacheza dhidi ya Galatasaray
mjini Gothenburg nchini Sweden, nchi anamotoka Ibrahimovic tarehe 30 Julai.
Kisha, watakutana na Everton mechi ya heshima kwa Wayne Rooney Old Trafford mnamo 3 Agosti
kabla ya kukutana na mabingwa wa Ligi ya Premia
kwa mechi ya Community Shield mnamo 7 Agosti.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top