
anachofanya ni kutoa kazi moja moja kila baada ya miezi mitatu.
Akihojiwa katika kipindi cha East Africa Breakfast
kinachorushwa na East Africa Radio, Lady Jaydee amesema album yake imekamilika na inaitwa
'Woman' hivyo hata huu wimbo mpya ni kutoka katika album hiyo.
Lady Jaydee amesema wazo la wimbo huo 'sawa
na wao' alilipata kutokana na maisha ya watu wake
wa karibu ambao amekuwa akiishi nao katika
maisha ya kila siku.
"Unajua mimi nina marafiki mbalimbali wa rika
zote, wapo walionizidi sana umri, wapo nalingana
nao na wengine ni wadogo zangu kabisa hivyo
muda mwingi napotoka nao au kujichanganya nao
ndipo nikapata wazo la wimbo huu 'Sawa na wao'.
"Kwani binadamu tunatofautiana. Saizi nimeamua
kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa kazi
moja kutoka kwenye album yangu hiyo ya
'Woman'. Alisema Lady Jaydee
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.