0
Serikali za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara zimelifunga Bwawa la Nyumba ya Mungu kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuepusha kutoweka
kwa viumbe hai wakiwamo samaki kutokana na kushamiri kwa uvuvi haramu.
Aidha, wakuu wa wilaya za Moshi, Mwanga na Simanjiro wametakiwa kusimamia maamuzi hayo
na kuchukua hatua kali za kisheria kwa
watakaokaidi agizo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki
alisema hayo wakati wa hafla maalumu ya
kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya mkoani
Kilimanjaro iliyofanyika mjini hapa, juzi.
Alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha
ujirani mwema baina ya mikoa hiyo kupitia wilaya
tatu zinazolizunguka bwawa hilo na kwamba
utekelezaji wa agizo hilo umeanza rasmi Julai
Mosi mwaka huu.
“Hali ya uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya
Mungu ni mbaya sana, mazingira yameharibiwa,
kuna athari nyingi zinajitokeza ikiwamo ya
kupungua kwa maji katika bwawa hilo na hii
huenda ikaathiri uzalishaji umeme na kutoweka
kwa viumbe hai....kama serikali hatuwezi
kuvumilia tena,” alisema Sadiki.
Pamoja na bwawa hilo, Sadiki alitaka wakuu wa
wilaya kusimamia agizo la Kamati ya Ushauri ya
Mkoa (RCC), kupiga marufuku misumeno ya
mnyororo, kwani imebaini ni adui mkubwa wa
misitu.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa
aliwakabidhi wakuu hao wa wilaya migogoro
mikubwa mitano iliyopo katika hatua mbalimbali za
utatuzi wake kupitia viongozi waliowatangulia na
kutaka kufuata sheria katika kuishughulikia.
Miongoni mwa migogoro aliyoitaja ni unaohusisha
jamii ya wafugaji wanaozunguka Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kampuni
inayohudumia uwanja huo ya KADCO kuhusu
umiliki wa eneo la ardhi.
Mgogoro mwingine ni wananchi wa wilaya ya
Longido mkoani Arusha na mwekezaji wa eneo la
utalii la Ndarakwai uliowahi kusababisha
kuchomwa moto kwa eneo hilo.



HabariLeo

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top