Chadema (Bavicha) la kufika Dodoma kusaidiana
na Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma
wameanza maandalizi ya kupokea vijana zaidi ya
2000.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini
Dodoma jana Malambaya Manyanya, Mwenyekiti
wa Bavicha Mkoa wa Dodoma alisema, kwa sasa
viongozi wa mkoa wameanza maadalizi ya
kuwapokea wageni wao ambao wanatarajiwa
kuanza kuwasili tarehe 21 na 22 Julai mwaka
huu.
Alisema, maadalizi hayo ni ya kuwapokea vijana
ambao watatoka katika mikoa yote ya Tanzania
kwa lengo la kutimiza tamko la Bavicha taifa la
kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
kuzuia mikutano na vikao vya CCM.
Alisema, kwa sasa mkoa tayari umeunda kikosi
cha kufanya kazi ya maadalizi ya ugeni huo
ambapo kwa nia njema utafika mjini Dodoma
kutekeleza kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia
vikao vyote na mikutano ya vyama vya siasa.
Alisema, maadalizi hayo ya kuwapokea vijana hao
ni pamoja na viongozi wa kitaifa wa Bavicha kwa
maana ya kutafuta mahali pa kulala na maandalizi
ya chakula.
“Wapo watu ambao wanadhani Bavicha wana
mpango wa kufanya fujo, sisi tunataka kurejesha
Demokrasia nchini na kutekeleza kauli ya mkuu
wa nchi.
“Tumekuwa tukiona jinsi mikutano ya Chadema
inavyozuiliwa, na sasa msimamo wa Bavicha ni
kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika
Julai 23 kwa lengo la kubadilishana uongozi kati
ya mwenyekiti wa sasa wa CCM na rais msitaafu
wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais John
Magufuli.
“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa
yote nchini watakaokuja Dodoma kusaidiana na
Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa
CCM.
“Kwa sababau mkuu wa nchi ametoa tamko la
kuzuia mikutano yote ya siasa ikiwa ni pamoja na
vikao vya ndani na mikutano ya hadhara hadi
2020.” Alisema Malambaya.
Alisema, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya
vyama vya siasa vya upinzani na mahafali ya
Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema
(CHASO) na kuwa, sasa wanashirikiana na polisi
kuhakikisha mikutano ya CCM haitafanyika.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.