0
JAJI Mkuu, Mohammed Chande Othman,
amesema Mahakama Maalumu ya Uhujumu
Uchumi na Ufisadi itaamua kesi kwa muda
usiozidi miezi tisa na kwamba itaanza na majaji
14.
Aidha, wameandaa kozi maalumu kwa majaji 14
watakaofanya kazi katika mahakama hiyo
itakayoanza Julai 11 hadi 15, mwaka huu, kwenye
Chuo cha Mahakama Lushoto mkoani Tanga, ili
kupeana mwongozo juu ya uendeshaji wa
mahakama hiyo.
Jaji Mkuu alisema, kesi zitakazoendeshwa katika
mahakama hiyo ni zile ambazo upelelezi wake
umekamilika ili uamuzi utolewe mapema. Kwa
mujibu wa Jaji Mkuu, dhamira ya Serikali ya
Awamu ya Tano ni kupambana na uhalifu huo.
Aliyasema hayo jana wakati alipotembelea
Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar
es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Mwalimu Nyerere vilivyopo katika Barabara ya
Kilwa, ambayo alisema yamezidi kuwa bora kuliko
miaka mingine.
Alisema baada ya sheria hiyo ya uhujumu
uchumi kupitishwa na Bunge, imekuwa na
marekebisho mengi na kuboreshwa kwa kiasi
kikubwa.
Jaji Mkuu alisema pia, hatua inayofuata ni Rais
kutoa idhini ya sheria hiyo na baadaye kupitishwa
kwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali ili ianze
kutumika.
Alieleza kuwa baada ya kutangazwa katika Gazeti
hilo la Serikali, Jaji anatakiwa kutunga kanuni
mbalimbali, mojawapo ikiwa ya kulinda mashahidi
kutokana na kuwa sheria hiyo inahusu makosa
makubwa na hatari ya ugaidi, rushwa na uhujumu
uchumi.
“Tuko mbioni kutunga kanuni hizo na kuhakikisha
mashahidi wanalindwa. Jengo la mahakama hii
litakuwa katika Chuo cha Sheria karibu na
Mlimani City na tayari tumepeleka wasajili
watendaji,” alisema.
Mwishoni mwa wiki, Jaji Mkuu huyo alisema kuwa
majengo ya mahakama hiyo yatakabidhiwa leo.
Kutokana na maelezo yake, Mahakama iko tayari
kuendesha divisheni hiyo, baada ya kukabidhiwa
majengo hayo.
Alisema wataanza kutoa semina kwa majaji na
watumishi wengine wa mahakama hiyo juu ya
namna divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli
zake.
Aidha, aliweka wazi kuwa hadi sasa hakuna kesi
hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba
itashughulikiwa na mahakama hiyo.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top