kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho,
licha ya kuwepo kwa msukumo mkubwa wa
kumtaka agombee.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya
habari, Mtatiro alisema kwa kipindi kirefu
amekuwa akipata msukumo kutoka kwa viongozi
wa chama hicho ngazi ya wilaya, wabunge,
wafuasi na makada wa chama hicho kumtaka
ashiriki katika kinyang’anyiro cha kugombea
nafasi ya uenyekiti.
“Katika kipindi chote cha misukumo hiyo
nimekuwa nikiwajibu wahusika wote kuwa “sina
nia ya kuchukua uongozi wa juu wa chama” kwa
sababu bado nahitaji muda wa kujiimarisha,”
alisema Mtatiro katika taarifa yake.
Alisema hata aliposhauri kuwa Mwenyekiti wa
zamani wa chama hicho, Profesa Ibrahim
Lipumba anapaswa kupumzika wapo walioona
kuwa anatumia nafasi hiyo kuutaka uenyekiti wa
CUF jambo ambalo alisema si kweli.
Aidha, Mtatiro alisisitiza kuwa hajawahi kuwa na
nia ya kuutaka uenyekiti wa CUF lakini hadi sasa
msimamo wake ni kuwa haungi mkono Profesa
Lipumba kurudi katika nafasi yake kwa sababu
siasa za sasa zinahitaji viongozi wapya na
wanaoweza kutazama mambo kisasa kwa
mahitaji ya kizazi kipya.
“... Na kwa sababu Profesa Lipumba anayo
heshima kubwa kwa CUF na watanzania, ni
muhimu zaidi alinde heshima yake na abaki kuwa
mshauri mkuu wa chama. CUF ya sasa inahitaji
mwenyekiti imara anayeweza kukisimamia chama
na kikajijenga lakini pia mwenye uwezo na
ushawishi wa kufanya siasa za ushirikiano na
haki,” ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo, Mtatiro alisema anawatakia kila la heri
wanachama wa CUF ili waweze kuchagua
mwenyekiti mzuri kwa ajili ya kukiendeleza
chama hicho, na kusisitiza kuwa jukumu lake
litaendelea kukisaidia chama katika masuala
mbalimbali ya kiushauri.
Chapisha Maoni