amewataka viongozi wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) kutokatishwa tamaa na
hali ya kisiasa nchini hususan marufuku za
mikutano yao ya kisiasa pamoja na misukosuko
mingine wanayopitia.
Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, ameyasema hayo jana jijini Arusha
alipokutana na Mameya na Wenyeviti wa
Halmashauri zinazoongozwa na Chama hicho.
Aliwataka wasiogope bali washikamane zaidi na
kutambua ukweli kuwa hakuna Serikali yoyote
duniani inayovipenda vyama vya upinzani.
Alisema kuwa Chama hicho kinatakiwa kujikita
katika kushikamana na wananchi zaidi kwani
uchaguzi wa mwaka jana ulionesha dhahiri kuwa
wana imani na vyama vya upinzani na hadi sasa
bado wananchi wana imani kubwa nao.
“Kuna uanaharakati na kuna siasa. Chama chetu
cha Chadema ni hodari sana, tume-graduate.
Tumevuka ngazi ya uanaharakati. Uanaharakati ni
mzuri lakini unafika mahali unavuka ngazi katika
kitu kingine ambacho ni chama cha siasa,”
alisema.
“Chama cha siasa kazi yake ni kukamata dola.
Hakuna kitu kingine duniani. Kwahiyo mnapokaa
hapa mnajipanga kukamata dola na sio kitu
kingine. Maandamano ni process tu, na sisi
tumekaa hapa kutafuta namna ya kukamata dola,
wanataka hawataki wanajua hilo.
"Na wenyewe watakazana kuzuia tusikamate dola.
Mliona walivyotufanyia kwenye uchaguzi, kwa
gharama yoyote. Na sisi kwa gharama yoyote
tutataka tuwanyang’anye dola na ndio tunakuwa
chama cha siasa,” aliongeza.
Alisema kuwa CCM wanahofu kwakuwa bado
wanakumbuka walichokipata wakati wa uchaguzi
mkuu uliopita na akawataka Chadema kutofanya
kazi kwa mazoea bali kukijenga chama kuanzia
ngazi za mashina na matawi.
Katika hatua nyingine, Lowassa aliwataka
Chadema pamoja na vyama vingine vya upinzani
kulinda Ukawa kwani ndio chanzo kikuu cha
mafanikio yao. Alisema wanapotofautiana wakae
chini na kutafuta ufumbuzi.
“Ndugu zangu tulinde umoja wetu na tuhakikishe
kuwa Ukawa inaendelea kuwapo hasa. Umoja
wetu ndio nguzo kubwa na tutumie busara
kukosoana. Tunapokosea tuache maneno ya
mitaani. Tuwalinde viongozi wetu ,” alisema.
Mwanasiasa huyo mkongwe alitoa wito kwa
viongozi hao wa halmashauri kuhakikisha
wanafanya kazi nzuri na kuwaletea maendeleo
wananchi ili wasione ‘bora CCM’.
Aliwataka kuhakikisha hawaangalii maslahi binafsi
bali maslahi ya wananchi na kujieupusha na
migogoro na viongozi wa CCM watakaotaka
kuwakwamisha katika shughuli zao.
Chapisha Maoni