0
Kocha wa Manchester United, Jose
Mourinho alifanya mkutano na waandishi
wa habari na kuweka wazi kuwa
mipango yao kwa sasa ni kusajili
wachezaji wanne na kati ya hao watatu
tayari wameshafanikiwa kuwasajili ila
anaamini mmoja atafanikiwa kumsajili
mapema pia bila kumtaja jina.
Mnamo Julai 7, 2016 taarifa kutoka Italia
zilizoripotiwa na Di Marzio ni kuwa
kocha Jose Mourinho anajiandaa
kumsajili staa wake wa 4 ambaye ni Paul
Pogba na tayari wameshafikia katika
makubaliano na klabu ya Juventus
anayoichezea nyota huyo.
Klabu ya Man U wamekubaliana na
Juventus dau la uhamisho wa Pogba,
ambaye atakuwa analipwa mshahara wa
paundi milioni 11.1 kwa mwaka, Pogba
kama akisajiliwa na Man United atakuwa
mchezaji wa nne kujiunga na Man United
chini ya Jose Mourinho, baada ya
kusajiliwa kwa Zlatan Ibrahimovic, Eric
Bailly na Henrikh Mkhitaryan.

Chapisha Maoni

 
Top