0

Julio ameeleza kuwa, hana mpango wa kuleta
wachezaji wa kigeni katika kikosi chake kwani
anaamini ni waganga njaa na uwezo wao ni duni
Kocha Mkuu wa Mwadui FC ya mkoani Shinyanga,
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amefunguka
kuwawachezaji wa kimataifa wanaokuja kucheza
soka nchini, wengi wao ni waganga njaa
kutokana na kutokuwa na uwezo wa juu kisoka.
Julio ambaye msimu uliopita alimaliza ligi timu
yake ikiwa katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu
Bara, ameeleza kuwa, hana pupa na usajili kwa
kuwa hahofii usajili wa timu kubwa na badala
yake anafanya mambo kwa mahesabu ili kuweza
kupata wachezaji wenye viwango.
Julio ameeleza kuwa, hana mpango wa kuleta
wachezaji wa kigeni katika kikosi chake kutokana
na kutambua kuwa wengi wao wapo kimaslahi
zaidi na wanakuja kuganga njaa Bongo huku
vipaji vyao vikiwa ni vya kawaida.
Akizungumza na gazeti la Championi Julio
alisema “Mimi nina mpango wa kupunguza kikosi
msimu huu ambapo msimu uliopita nilisajili
wachezaji 33 lakini kwa sasa nitasajili wachezaji
23 kati ya hao, makipa watatu na wachezaji wa
ndani 20.
“Sina haja ya kusajili maprofesheno kwani
asilimia kubwa wapo hapa kwa ajili ya kuganga
njaa tu, hawana kiwango chochote. Wachezaji
ambao ni maprofesheno ambao wapo vizuri
wanaocheza ligi kuu ni Ngoma (Donald),
Tchetche (Kipre) na Wawa (Pascal) waliobakia
wote hakuna kitu, wanaganga njaa tu,” alisema
Julio.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top