Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub
‘Cannavaro’ amewataka wapinzani wao katika
mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika,
Medeama kujiandaa na kipigo kutokana na
maandalizi makali waliyofanya kwa wiki mbili
kujiandaa na mchezo huo.
Yanga itashuka Uwanja wa Taifa kesho
kuwakaribisha Medeama ya Ghana, ukiwa ni
mchezo wa tatu wa Kundi A.
Katika mahojiano na gazeti la HabariLeo,
Cannavaro aliyekosa mechi zote mbili za awali
ambayo timu yake ilipoteza, alisema hawapo tayari
kuona wanafungwa mchezo huo ndiyo sababu ya
kupania kuhakikisha wanaibuka na ushindi ambao
utawaweka kwenye nafasi nzuri ya kucheza nusu
fainali za michuano hiyo.
“Mimi nawaomba Medeama wajiandae kwa kipigo
kwa sababu hatupo tayari kupoteza mchezo
mwingine, tumefanya maandalizi ya kutosha
kuhakikisha tunarekebisha matokeo yetu na
tumepanga kuanza nao hao Waghana tukiamini
hakuna linaloshindikana,” alisema Cannavaro.
Mkongwe huyo alisema baada ya kupoteza mechi
mbili za awali dhidi ya MO Bejaia ya Algeria na TP
Mazembe ya Congo DR, wamegun- dua makosa
yao na benchi lao la ufundi tayari limeyafanyia kazi
na sasa wapo tayari kubadili mwenendo wao kwa
kushinda michezo yote iliyopo mbele yao.
Alisema anajua wapinzani wao nao wamejipanga
kutaka kupata ushindi, lakini watawasamehe kwa
sababu kupoteza michezo miwili ya awali
imewaumiza na wasingependa matokeo hayo
kuwazoea kwani kusudio lao ni kucheza fainali.
Yanga inaburuza mkia kwenye kundi hilo ikiwa
haina alama yoyote baada ya kufungwa mechi zote
mbili za awali, na endapo itapoteza tena mchezo
huo itapoteza matumaini ya kufika fainali kama
ilivyokusudia. Tayari baadhi ya wachezaji wa
wapinzani wao Medeama waliwasili nchini jana, na
kundi lingine likitarajiwa kuwasili leo tayari kwa
mechi hiyo.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.