0

Wakata miwa wa mjini Morogoro Klabu ya
Mtibwa Sugar imefanikiwa kuinasa saini ya
mshambulijai wa Timu ya Taifa ya
Tanzania na klabu ya Mwadui FC Rashid
Mandawa.
Mandawa amesaini mkataba wa mwaka
mmoja kukipiga katika klabu hiyo ya
Manungu Complex habari ambayo
imethibitishwa na Mtendaji mkuu wa
Mtibwa Sugar, Jamal Bayser ambaye
amemtaja pia beki wa Ndanda FC Cassian
Ponera kusajiliwa na Mtibwa Sugar kuziba
nafasi iliyoachwa na Endrew Vicent
aliyetimkia Yanga.
Mtibwa Sugar iliyomaliza katika nafasi ya 4
katika msimamo wa ligi hiyo msimu
uliopita itajengwa upya na kocha Salumu
Mayanga ambaye msimu uliopita alikua
akiinoa Prisons ya Mbeya.
Mtibwa Sugar mabigwa wa 1999 na 2000
wa Ligi ya Vodacom Tanzania wameanza
maandalizi ya msimu ujao wakiweka kambi
yao Jijini Dar es Salaam kabla ya kurudi
Manungu kwenye kambi yao ya siku zote.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top