0

Mjerumani Leroy Sane anaonekana kukubali
kutimkia Manchester City baada ya kuripotiwa
kuwa amekubali vigezo binafsi
Mshambuliaji huyo wa Schalke 04 ambaye
alikuwa katika kikosi cha Ujerumani cha Euro
2016, ametajwa mara nyingi kukaribia kutua
katika Ligi Kuu ya Uingereza miezi ya hivi
karibuni.
Habari zinadai kuwa nyota huyo mwenye umri wa
miaka 20 amekubali kujiunga na kikosi cha Pep
Guardiola kwa mkataba wa miaka minne lakini
bado klabu haijatoa ofa rasmi.
Kwa mujibu wa Bild, City wanaandaa kitita cha
paundi milioni 46.5 ambacho kinaaminika kuwa
kiasi ambacho Schalke wanakihitaji.
Iwapo City wataamua kusubiri hadi msimu ujao,
Sane atagharimu miamba hao wa Manchester
kiasi cha paundi milioni 31.3, lakini inaaminika
mchezaji huyo anatamani zaidi kujiunga na klabu
hiyo ya Uingereza sasa.
Sane amefunga mabao tisa katika mechi 42
alizocheza Schalke katika michuano yote msimu
uliopita.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top