Kocha mpya wa Azam FC, Zeben Hernandez
ameuomba uongozi wa klabu hiyo kumpatia
mechi moja ya kirafiki ili kujua amefikia wapi
tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo
Kocha mpya wa Azam FC, Zeben Hernandez
ameuomba uongozi wa klabu hiyo kumpatia
mechi moja ya kirafiki ili kujua amefikia wapi
katika mazoezi ya wiki moja tangu alipoanza
kuifundisha timu hiyo kujiandaa na msimu ujao.
Hernandez ameiambia Goal , katika wiki moja
amewafundisha vijana wake mambo mengi hivyo
asingependa kuendelea mbele hadi kujua
wachezaji wake wameyapokeaje mafundisho hayo
aliyowapa.
“Mchezo wa kirafiki na timu yoyote itakuwa ni
kipimo kizuri kwangu kujua nilipofikia kwasababu
kimtazamo vijana wanaonekana wameanza kuwa
tayari lakini hilo haliwezi kunipa uhakika hadi
nipate mchezo wa majaribio ,”amesema
Harnandez.
Tayari uongozi umeichagua Asanti United, kuwa
ndiyo timu watakayocheza nayo mchezo huo wa
kirafiki kwasababu nayo ni ipo kwenye maandalizi
ya kujiandaa na Ligi daraja la kwanza Tanzania.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.