0
Safu ya ushambuliaji msimu uliopita ilimtegemea sana Hamis Kiiza na pindi asipokuwepo timu ilikosa mbadala sahihi wa kuziba pengo lake
Miaka 4 sasa imepita bila ya Simba kuchukua
ubingwa wa ligi kuu bara na kuiwakilisha nchi
katika michezo ya kimataifa, timu
hiyo amekabiziwa Mkameruni Joseph Omog kwa
ajili ya kurudisha makali yake ya awali.
Je! Nini anatakiwa kufanya ili kuipaisha Simba
msimu ujao ili kuirejeshea heshima yake ya awali?
Maandalizi mazuri ya msimu mpya
Tayari Simba ipo Morogoro kwa ajili ya msimu mpya ligi kuu bara, timu nzuri hujengeka kwenye
kipindi cha mapumziko, Joseph Omog anahitaji
kutumia muda huu vizuri kuiandaa timu yake
vizuri kimwili na kiakili na ndio muda sahihi wa
kupata kikosi cha kwanza kabla ya msimu kuanza.

Usajili
Timu zipo kwenye kipindi cha usajili, Omog
amekuta timu tayari imeshafanya baadhi ya
usajili kwa wachezaji wa ndani kama Kichuya,
Muzamili Yasin, lakini bado anayo nafasi ya
kuongeza wachezaji zaidi kwenye timu hasa
wachezaji wa kigeni, atumie vizuri zile nafasi
saba za kigeni kusajili wachezaji wenye uwezo
mkubwa kuliko wazawa.
Kurudisha umoja kwenye timu
Moja ya sababu kubwa iliyopelekea Simba
kufanya vibaya msimu uliopita ni kutokuwa na
umoja baina ya wachezaji na benchi la ufundi na
viongozi kwa ujumla mfano msimu uliopita kocha
mkuu Kerr kutokua na umoja na msaidizi wake
Matola hadi Matola kuamua kuachia ngazi, moja
ya changamoto aliyo nayo Omog ni kutengeneza
umoja ndani ya timu na viongozi, hii ndo itakuwa
silaha kubwa kwake kufanya vizuri kwenye ligi
kuu.
Kuimalisha safu ya ushambuliaji
Safu ya ushambuliaji msimu uliopita ilimtegemea
sana Hamis Kiiza na pindi asipo kuwepo timu
ilikosa mbadala sahihi wa kuziba pengo lake,
moja ya silaha ya Yanga kwa msimu uliopita ni
safu bora ya ushambuliaji ndo ilipelekea kutetea
taji lake uwezo wa kufunga kwa Tambwe, Ngoma
na Msuva. Bwana Omog anatakiwa kuunda safu
bora ya ushambuliaji ambayo haimtegemei mtu moja.
Nidhamu
Swala la nidhamu ni changamoto kubwa sana
kwenye klabu ya Simba, msimu uliopita matukio
ya nidhamu baina ya wachezaji na benchi la
ufundi yalikuwa mengi mno kwa kipindi tofauti tofauti baadhi ya wachezaji walisimamishwa kwa
utovu wa nidhamu kama Kiiza, Hasan Isihaka,
Ajibu, Majabvi. Omog anastahili kurudisha
nidhamu ndani ya timu ili kufanikiwa kuunda timu bora, nidhamu mbovu haiwezi jenga timu bora.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top