mshambuliaji Cristiano Ronaldo kabla ya
fainali ya michuano ya Euro 2016 kati ya
Ufaransa na Ureno kuanza. Ila hali
ilibadilika baada ya Ronaldo kuumia na
kulazimika kuondoka uwanjani! Kwa
wengi, kitumbua cha Ureno kilikuwa
kimeingia mchanga. Lakini, baadaye
kulijitokeza shujaa mwingine.
Mchezaji Eder nusura aumie muda mfupi
baada ya kuingia uwanjani. Mashabiki
wengi wa soka duniani, walimfahamu
mshambuliaji mtata, Eder, aliyefunga bao
la ushindi dakika ya 109 na kuzamisha
ndoto ya Wafaransa uwanja wa Stade de
France, Paris. Eder aliingia nafasi ya
kiungo wa kati, Renato Sanches.
Uliyajua haya mambo muhimu kumhusu
Eder? Jina lake kamili ni Éderzito António
Macedo Lopes, Macedo likiwa jina la
ukoo wa mama yake na Lopes jina la
ukoo wa baba yake. Eder alizaliwa nchini
Guinea-Bissau, taifa lililotawaliwa na
Wareno hadi lilipojinyakulia uhuru
mwaka 1974.
Jamaa ana umri wa miaka 28 na
anasema Ronaldo alimwambia angefunga
bao. “Alinipa moyo na nguvu, na hilo
lilikuwa muhimu!” Kimo cha Eder ni futi
6 na inchi 3. Alihamia Ureno akiwa
mtoto, soka yake ya kulipwa alianza
kucheza mara ya kwanza klabu ya
Academica 2008 kabla ya kujiunga na
klabu ya Braga miaka minne baadaye
ambapo aliwika sana.
Pia, alichezea klabu ya Swansea mwaka
2015 baada ya kununuliwa kwa £5
milioni kutoka Braga. Mechi yake ya
kwanza Ligi ya Premier ilikuwa sare ya
2-2 dhidi ya mabingwa watetezi wa
wakati huo Chelsea alipoingia nafasi ya
Bafetimbi Gomis. Hakufunga bao lolote
Swansea na akatumwa klabu ya Lille ya
Ufaransa inayocheza Ligue 1 kwa mkopo
kipindi kilichosalia cha msimu. Eder
alijiunga rasmi na Lille kwa mkataba wa
kudumu Mei mwaka huu baada ya
kuwasaidia kufuzu kwa Europa League.
Kwenye uchezaji wake Ligi Kuu ya
Ureno, alicheza jumla ya mechi 143 na
kufunga mabao 38. Eder amechezea
timu ya taifa ya Ureno tangu 2012 na
aliwachezea Kombe la Dunia 2014.
Alifungia Ureno bao lake la kwanza la
kimataifa mechi yake ya 18, mechi ya
kirafiki dhidi ya Italia katika uwanja wa
Stade de Geneve, Juni 2015.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.