0
MSHAMBULIAJI wa kimataifa
wa Tanzania, Mbwana Ally
Samatta amefunga bao lake
la kwanza katika michuano
ya Europa League usiku huu,
timu yake, KRC Genk ikiilaza
2-0 Buducnost ya
Montenegro Uwanja wa
Luminus Arena mjini Genk.
Katika mchezo huo wa
kwanza wa Raundi ya Pili ya
mchujo, Samatta alifunga bao
la pili dakika ya 79, baada ya
kiungo kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) Neeskens Kebano
kufunga la kwanza kwa
penalti dakika ya 16.
Genk sasa itatakiwa kwenda
kuulinda ushindi wake katika
mchezo wa marudiano Julai
21, Uwanja wa Pod Goricom
mjini Podgorica ili kusonga
mbele Raundi ya Tatu ya
mchujo.
Ratiba ya Raundi ya Tatu ya
mchujo itapangwa leo na
mechi za kwanza zitachezwa
Julai 28 wakati marudiano
yatakuwa Agosti 4, mwaka
huu.
Timu zitakazoshinda
zitakwenda hatua ya mwisho
ya mchujo kuwania
kupangwa kwenye makundi,
ambako sasa vigogo kama
Manchester United ya
England wataanzia huko.
Kikosi cha KRC Genk
kilikuwa: Bizot, Castagne,
Dewaest, Kumordzi, Uronen,
Ndidi, Buyens/Heynen dk73,
Kebano/Karelis dk76, Bailey,
Buffalo na Samatta/Trossard
dk87.
Buducnost Podgorica :
Dragojevic, Vusurovic (84
'Camaj), Mitrovic, Vukcevic,
Radunović, Pejakovic/Seratlic
dk74 Raickovic/Janketić
dk59, Hoko, Đalović,
Mirkovic na Raspopovic

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top