0

Manchester United imepata ushindi wa mabao 2-0
kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Wigan.
Katika mchezo huo, Luke Shawa alirejea dimbani
mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa takribani
miezi 10.
Shaw alivunjika mguu mwezi September mwaka
jana.
Mabao ya United yalifungwa na Will Keane na
Andreas Pereira.
Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly waliichezea
United kwa mara ya kwanza wakati Ibrahimovic,
Rooney, Smalling na Rashford bado wako likizo
kutokana na ushiriki wao kwenye michuano ya
Euro 2016 iliyomalizika umapili iliyopita.
Mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa
hazijafungana, kipindi cha pili Mourinho alifanya
mabadiliko kwa kuingiza wachezaji saba, Keane na
Juan Mata wakiwa miongoni mwao.




Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top