Young Africans 1-1 Medeama
MPIRA UMEKWISHAAA
-Chirwa anaingia na kupiga krosi nzuri
kabisa, lakini Ngoma anaonekana kutokuwa
na nguvu ya kumalizia
-Ngoma anaingia vizuri, anakwenda
anaanguka mwenyewe akionekana kuwa
amechoka
-Yanga wanafanya kosa kosa lka mwaka,
Abbas Mohammed aliyeingia kipindi cha pili
anabaki yeye na kipa Dida lakini
anashindwa kufunga, hii ni bahati kubwa
kwa Yanga
-Yanga wanafanya shambulizi tena lakini
Medeama wanaokoa
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 90, Medeama wanafanya shambulizi kali
ndani ya eneo la hatari la Yanga
wakigongeana vizuri lakini Bossou anaokoa
na Dida anadaka vizuri
DK 87 hadi 89, Yanga wanafanya
mashambulizi, lakini wanaonekana kuishiwa
maarifa. Maana wanapiga krosi ambazo
hazina manufaa lakini wanaendelea kupiga
krosi tena na tena
Dk 86, Yanga wanajichanganya, Twite
anampa adui mpura, anaingia vizuri Kwame
na kupiga shuti, hata hivyo anashindwa
kulenga lango
Dk 85, Medeama bado wanaonekana
kupoteza muda wakitaka sare huku Yanga
wakionekana kuwa na presha wakitaka
kupata bao la pili
Dk 84, Mahadhi anajaribu kuwatoka mabeki
wa MEdeama lakini Adade anawahi na
kuokoa
Dk 82, Niyonzima anapokea pasi ya
Mahadhi, anageuka haraka na kupiga shuti
kali, lakini mabeki Medeama wanakoa tena
Dk 80, Yanga wanagongeana vizuri,
Mahadhi anauwahi mpira wa Niyonzima na
kupiga shuti kali, kipa Medeama
anaonyesha ujuzi na kuokoa tena
SUB Dk 77, Yanga wanamtoa Joshua na
nafasi yake inachukuliwa na Haruna
Niyonzima. Hii maana yake Twite anashuka
kwenda kucheza namba tatu, Kamusoko
anashuka sita na Niyonzima anakwenda
nane
SUB Dk 76, Juma Mahadhi anaingia
kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe
Dk 73, krosi nyingine safi kabisa ya Juma
Abdul, mabeki Medeama wanajichanganya
lakini hakuna mtu pale, wanaokoa tena
Dk 73, unaweza ukadhani utani, Yanga
wanapoteza nafasi nyingine tena ya wazi
kabisa. Ngoma ndani ya eneo la 18, kipa
ndiyo pekee mbele yake, anashindwa
kufunga kwa kichwa
Dk 70, Kamusoko anaanchia shuti kali
kabisa, kipa Medeama anaonyesha ujuzi
hapa na kuutoa, kona. Yanga wanapiga
lakini haina madhara
Dk 69, Yanga wanamuacha Kwake aingie
peke yake, hayuko mbali sana na lango
anapiga shuti lakini linapita juu ya lango la
Yanga
Dk 65, Msuva anakwenda kuzozana na kipa
wa Medeama akitaka mfuko wa kipa
aliouweka ndani ya lango uondolewe,
mwamuzi anamsikia na kumwamuru kipa
huyo aende kuutoa na kuuweka nje ya
lango
Dk 64, mpira umesimama takribani dakika
moja,beki Aidoo wa Medeama akiwa chini,
akidai alichezewa rafu
Dk 62 Yondani anapanda na kupiga pasi
nzuri, Yanga wanafanya shambulizi na krosi
nzuri ya Juma Abdul lkakini Medeama
wanaokoa tena
Dk 59, Juba Abdul anaingia na kupiga krosi
safi kabisa, Ngoma anaunganisha kwa tik
tak lakini kipa anaokoa vizuri kabisa
Dk 54 hadi 57, Yanga wanaonekana kutulia
vizuri na kucheza pasi mpira wakiwa nao,
lakini bado hawajafanya shambulizi kali
hata mara moja
Dk 52, Tambwe anaingia vizuri tena,
anampa mpura MSuva lakini Medeama
wanaokoa vizuri
Dk 50, Medeama wanaingiza mpira mzuri
ndani ya lango la Yanga lakini Yondani
anawahi na kuokoa
Dk 48, Tambwe anapoteza nafasi nzuri
kabisa, anabaki yeye na kipa na kushindwa
kufunga, nini hiiii
Dk 46 Mpira unaanza taratibu lakini Ngoma
anamwangusha mshambulizi wa Medeama
MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Yanga wanaanza kushambulia tena,
lakini bado hakuna mashambulizi makali
kwakuwa aina yao ya uchezaji ni kupiga
mipira mirefu na Ngoma amethibitiwa
Dk 42, Twite anamwangusha mshambuliaji
wa Medeama ambaye alimtoka Bossou kwa
kasi kubwa, lakini mwamuzi anamsamehe
Dk 39, Bossou anaanguka wakati akiwania
mpira na Kwame, lakini pamoja na janja
yake analambwa kadi ya NJANO.
Dk 37, Medeama wanapata kona,
wanachonga na wao wanauwahi na kupiga
na unatoka kidogo nje ya lango la Yanga.
Hili ni kosa kama lililozaa bao la kwanza
Dk 35, Chirwa anamgeusa Aidoo wa
Medeama nakubaki yeye na kipa lakini
anampa mikononi
Dk 33, Tambwe anapiga kichwa tena lakini
unakuwa mpira lahisi kwa kipa wa
Medeama
Dk 32, Oscar Joshua anaingiza krosi safi
kabisa lakini moira unampita Tambwe
Dk 31, Dida anajitokeza na kudaka vizuri
mbele ya Kwame. Kinachoonekana Yanga
wana tatizo la kiungo na wanapoteza mipira
mipingi sana
Dk 29, Juma Abdul ananusurika kulambwa
kadi ya njano baada ya kumchezea kindava
Kwame wa Medeama
Dk 28 Yanga wanaonekana kuamka krosi ya
Juma Abdul lakini Medeama wako makini
zaidi
Dk 22 hadi 25, Medeama wanaonekana
kushambulia zaidi kuliko Yanga na
wakicheza kwa kujiamini
Dk 20, Medeama wanafanya shambulizi
jingine na Yondani anajitokeza na kuokoa
GOOOOOO Dk 17, Benard Danso anaifungia
Medeama bao la kusawazisha baada ya
kuunganisha mpira wa kona akiwa mbele
ya Bossou
Dk 12 hadi 15, Medeama wanaonekana
kuchezea zaidi upande wa Yanga na
wanalazimika kuwa makini
Dk 11, Yanga wanalazimika kuokoa tena
baada ya Kwaeme kumpa pasi nzuri Adade
lakini hata hivyo hawakuwa makini
DK 8, MEdeama wanaingia vizuri kwenye
lango la Yanga, kinachoonekana hapa ni
kama Yanga wanafanya mzaha. Yanga
waliokoa lakini Yondani akaanguka na
Medeama wanapata nafasi aya kupiga shuti
Dk 4, Kamusoko anaingia vizuri tena na
kutoa paso lakini Tambwe anashindwa
kumalizia
GOOOOOOOO DK 1 Ngoma anaipatia Yanga
bao safi baada ya Msuva kuingia na kupiga
pasi safi kabisa
KIKOSI 01. Deo Dida
02. Juma Abdul
03. Oscar Joshua
04. Kelvin Yondani
05. Vicent Bossou
06. Mbuyu Twite
07. Simon Msuva
08. Thabani Kamusoko
09. Donald Gnome
10. Amissi Tambwe
11. Obey Chirwa
Chapisha Maoni