thamani yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba.
Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya
kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa
kwake 2011.
United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn).
Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na
Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn).
United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa sana na mkataba wao wa £750m
na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya.
Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika 25
bora.
Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na
Liverpool (41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha
hiyo.
Chapisha Maoni