0
Akiongea baada ya kukamilika uhamisho,
Mkhitaryan alisema, “Nasikia fahari mno
kujiunga na Manchester United, hii ni
ndoto yangu kutimia!”
Naye meneja wa Man United, Jose
Mourinho, alieleza, “Henrikh ni mchezaji
mwenye kipaji kikubwa ambaye
amekuwa kwenye fomu nzuri mno kwa
klabu na nchi yake. Ni mchezaji mahiri
wa kitimu mwenye uwezo mkubwa,
uelewa na jicho safi la kufunga magoli.
Nimefurahi ameichagua United. Naamini
ataleta msukumo kwenye timu kwani
uchezaji wake ni sahihi kwa Ligi Kuu.”
Klabu ya soka ya Manchester United
imetangaza rasmi kuwa Henrikh
Mkhitaryan amekamilisha uhamisho
wake kutoka Borussia Dortmund! Kiungo
huyo amesaini mkataba wa miaka minne
na Man United ambao una nyongeza ya
mwaka mmoja.
Mkhitaryan
Mchezaji Mkhitaryan, mwenye miaka 27,
aliichezea Dortmund mechi 140 na
kufunga bao 41 tangu ajiunge nao
mwaka 2013. Msimu uliopita, Mkhitaryan
aliifungia Dortmund bao 23 na
kutengeneza bao 32 na kuteuliwa kuwa
ndiye mchezaji bora wa Bundesliga kwa
msimu wa 2015/16 na pia kuwemo
kwenye timu ya msimu iliyoteuliwa na
chama cha kutetea haki za wachezaji wa
kulipwa huko Ujerumani, VDV.
Kiungo huyu ndiye mfungaji bora katika
historia ya timu ya taifa ya Armenia
akiwa na bao 19 katika mechi 59 tangu
aanze kuichezea Januari 2007 na pia
ndiye kepteni wa timu hiyo huku pia
akizoa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
wa Armenia kwa mara 5.

Chapisha Maoni

 
Top