Uingereza Mo Farah ameanza kujiandaa
kwa ajili ya kujifua kwa mara ya mwisho
kabla ya kushiriki mashindano ya
Olimpiki yatakayofanyika Agosti, mwaka
huu kule Rio de Janeiro, Brazil ambapo
atakuwa na jukumu la kutetea mataji
yake.
Mo Farah atakimbia umbali wa mita
5,000 katika mashindano ya Muller
Anniversary yatakayofanyika jijini London
Julai 23, mwaka huu. Mwanariadha huyo
ni bingwa wa mbio za mita 5,000 na
mita 10,000 na anatarajiwa kutetea
ubingwa wake huo kwenye mashindano
hayo yanayosubiriwa kwa hamu.
Chapisha Maoni