0
Mchezaji bingwa wa mbio za Olimpiki za
walemavu, Oscar Pistorius, anaweza
kuwa miongoni mwa wanariadha
watakaoshiriki michuano ya Olimpiki,
Tokyo, nchini Japan kama akiomba
msamaha kwa jamii ili kuwa sehemu ya
mashindano hayo.
Mkurugenzi mkuu wa michuano ya
Olimpiki nchini Afrika Kusini, Tubby
Reddy, anasema kwamba mwanariadha
huyo anaweza kutumikia mwaka mmoja
tu akiwa jela na baadaye kutoka na
kuendelea na mazoezi ya kujifua na
michuanoa hiyo.
Ndugu Reddy anasema kwamba
hakutakuwa na tatizo kwa mwanariadha
huyo kurejea kwenye kikosi cha
wanariadha watakaokwenda Tokyo kwa
ajili ya kuliwakilisha taifa lake kwenye
michuano hiyo. Anasema kwamba,
mwanariadha huyo anatakiwa kurudi na
kuomba radhi kwa jamii ikiwa ni pamoja
na kuishi maisha ya kawaida kama raia
mwingine ndani ya Afrika Kusini na
kudai kuwa hakuna sheria inayomzuia
mwanariadha huyo kujumuika na jamii
yake.
Mtuhumiwa huyu Pistorius anatakiwa
kufanya hivyo kutokana na kuigawa jamii
ndani ya Afrika Kusini kwa kuwa wapo
ambao hawatafurahi kwa kitendo cha
yeye kuwa huru lakini wengine watakuwa
na furaha. Reddy anasema kwamba,
Pistorius anaweza kutumikia kifungo cha
nje baada ya mwaka mmoja kuwa jela
na kuwa na muda mrefu wa kujiandaa
kabla ya michuano hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top