Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, amesema
kuwa mchezo wao unaofuata wa kombe la
Shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama ya
Ghana ni wa kufa na kupona.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ngoma, alisema
kuwa hawana chaguo lingine zaidi ya ushindi
kwenye mchezo huo muhimu.
"Watu waanze kutuhukumu au kutucheka baada ya
mchezo wetu na Medeama, ni lazima ushindi kwa
sababu bila kufanya hivyo tukuwa
tumejiangamiza," alisema Ngoma.
Alisema kuwa mashabiki wasiwe na shaka kwa
kuwa wamejiandaa vyema kushinda mchezo huo.
"Watuamini tu,tumepoteza michezo miwili na kwa
sasa hatufikilii hilo kutokea tena, tutacheza na
Medeama huku tukifahamu kabisa ushindi ni
muhimu kwetu," alisema Ngoma.
Nyota huyo raia wa Zimbabwe, ameshindwa
kuzifumania nyavu katika michezo miwili hatua ya
makundi waliyocheza mpaka sasa.
yanga imepoteza michezo yake miwili kwa
kufungwa goli 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Posted Africa Newss
Chapisha Maoni