Kaya wapeperusha bendera ya Uturuki
kwenye mashindano ya riadha barani
Ulaya. Wanariadha hawa wawili
wanaowakilisha Uturuki kwenye
mashindano ya riadha barani Ulaya
walifanya vyema na kuweza kuondoka
na nishani katika mbio za mita 10,000
kwenye kitengo cha wanaume.
Polat Kemboi Arikan aliweza kushinda
nishani ya dhahabu kwenye mashindano
hayo yanayoendelea katika mji mkuu wa
Amsterdam nchini Uholanzi.
Mwanariadha mwenzake Ali Kaya naye
aliweza kushinda nishani ya fedha baada
ya kumaliza kwenye nafasi ya pili.
Kwa matokeo hayo, hadi kufikia sasa
Uturuki imeweza kukusanya nishani 3 za
dhahabu, 2 za fedha na 2 za shaba.
Chapisha Maoni