es Salaam maarufu Sabasaba, yanatarajiwa
kufunguliwa leo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame,
ikiwa ni maonesho ya kwanza ya mpango wa pili
wa miaka mitano ya ujenzi wa uchumi wa viwanda
nchini.
Kutokana na uzinduzi, Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Charles Mwijage amewahimiza
wananchi kufika kujifunza uanzishaji wa viwanda
vidogo, kati na vikubwa.
Akizungumzia ufunguzi huo, Mwijage alisema
katika maonesho hayo wenye ndoto za kuanzisha
viwanda hawana budi kufika kujifunza namna ya
kujenga viwanda kwa fedha kidogo wakiungwa
mkono na taasisi za kifedha.
Alisema maonesho hayo yanayoshirikisha nchi
zaidi ya 30 yatatumika kurasimisha biashara kwa
kutumia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA) kwa muda mfupi.
“Brela itakuwepo kuonesha kuwa Tanzania ina
uwezo wa kusajili kampuni kwa muda mfupi
isipokuwa mtu awe na nakala muhimu,” alisisitiza.
Alisema katika kuonesha maonesho hayo
yamejikita kujengea uwezo Watanzania kuanzisha
viwanda vinavyozalisha bidhaa bora kuna banda
maalumu lenye wataalamu wa viwanda na
uwekezaji watakaotoa maelekezo ya viwanda na
uwekezaji.

Chapisha Maoni