0
Mchezaji na kinda wa Mabingwa wapya wa Ulaya, Ureno Renato Sanches ametajwa kuwa mchezaji bora chipukizi katika mashindano ya Euro mwaka
huu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18, ana uwezo wa hali ya juu kabisa ameshinda tuzo hiyn na kuwashinda wenzake Kingsley Coman wa
Ufaransa na Mreno mwenziwe Raphael Guerreiro.
Zawadi hizo ambazo zilikuwa maalum kwa wale wote waliozaliwa baada ya January 1 1994, zilitolewa na jopo la Wataalamu wa masuala ya
Kiufundi wa UEFA lililokuwa likiongozwa na Lupescu.
Wengine waliokuwa kwenye jopo hilo ni Sir Alex Ferguson na Alain Giresse.
Sanches alianza kuonesha uwezo wake pale tu alipopewa nafasi kwenye mchezo dhidi ya Poland
na kuonesha kiwango bora kabisa
kilichomshawishi kocha wake kumuanzisha
kwenye mechi zilizofuata.
Sanches alifunga goli lake la kwanza kwa timu
yake katika mchezo dhidi ya Poland na kumfanya kuwa mchezaji wa tatu kijana kucheza mchezo wa fainali ya Euro mwaka huu.
Alikuwepo kwenye mecho zote muhimu ambazo
Ureno walipata ushindi….dhidi ya Wales ambapo walishinda 2-0 na jana dhidi ya Ufaransa na kumfanya kushinda tuzo hiyo katika umri mdogo
zaidi wa miaka 18 na siku 328.
Kinda huyo mzaliwa wa Lisbon, ambaye kwenye dirisha hili la usajili amejiunga na Bayern München
akitokea Benfica kwa ada ya awali ya uero mil 35, alianza msimu wa 2015/16 akiwa na timu B ya Benfica na kushiriki katika Michuano ya Ligi ya
Vijana ya UEFA, Michezo ya kufuzu Michuano ya
Ulaya kwa vijana chini ya miaka 19 na vile vile LigiI a Mabingwa Ulaya kabla ya kupata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Ureno kwa mara ya
kwanza March 25 mwaka huu.
Renato Sanches na Kingsley Coman msimu ujao
watakuwa wote kunako klabu ya Bayern huku Raphael Guerreiro naye atakuwa nchini Ujerumani lakini akikipiga kunako klabu ya Borussia Dortmund.

Chapisha Maoni

 
Top