0
Nyota wa timu ya taifa ya Wales, Gareth
Bale amempa sifa staa mwenzake wa
Real Madrid, Cristiano Ronaldo akisema
kuwa ni mkali wa mabao, baada ya
kuifungia timu yake ya Ureno katika
ushindi wa mabao 2-0, dhidi yao katika
mchezo wa nusu fainali za Euro 2016.
Kabla ya mtanange huo kufanyika,
ulikuwa ukizungumziwa na wengi kuwa
unaikutanisha miamba miwili hatari,
lakini baada ya kufanyika, alikuwa ni
Ronaldo ambaye aliibuka kidume.
Nyota huyo aliibuka kidume dakika ya 50
wakati alipofunga bao kwa mpira wa
kichwa na kushuhudiwa akifikia rekodi
ya nyota wa zamani wa timu ya taifa ya
Ufaransa, Michael Platini kwa kufunga
mabao tisa katika fainali hizo za Ulaya
na huku nyota huyo akiwa
amemtengenezea bao Nani dakika tatu
baadaye.
Gareth Bale
Bale alisema kuwa nyota huyo ni mkali
wa mabao na ndio maana alifunga tena.
“Lakini sio kwamba namzungumzia yeye
peke yake bali na kwetu sisi kwa ujumla
tumecheza vizuri na najivunia kwa hili.
Tunatakiwa kujivunia mafanikio ambayo
tumeyapata katika mashindano haya,”
alisema staa huyo. “Tungependa
kuwashukuru mashabiki kwa msaada
waliotupa na ndio maana tumefikia
hapa,” aliongeza nyota huyo. Katika
mchezo huo wa usiku wa kuamkia juzi,
Wales walionekana kuwa sawa na
wapinzani wao na Bale anasema kuwa
kiwango walichokionyesha kilikuwa ni
cha hali ya juu. “Walipata bao kipindi
cha kwanza na sisi tulikosa bahati
kipindi cha pili,” aliongeza. “Ila tulijaribu
kurudi katika mchezo na ndio maana
tukapambana hadi dakika ya mwisho,”
aliongeza tena staa huyo.

Chapisha Maoni

 
Top