Mlinda mlango wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida' amesema hawawezi kuidharau timu ya Medeama katika mchezo wao utakaopigwa
Jumamosi ya Julai 16 mwaka huu.
Dida amesema, Medeama ni timu kubwa na
ngumu tofauti na watu wanavyoifikiria lakini
kikubwa watahakikisha wanapambana ili kuweza
kuibuka na ushindi.
Dida amesema, anaamini mchezo huo utakuwa na
ushindani lakini kutokana na maandalizi ya
uhakika wanayoendelea nayo wanaamini nafasi ya
kufanya vizuri bado ipo.
Yanga na Medeama zitashuka dimbani kupambana
katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho
litakalopigwa Uwanja wa Taifa jijini dar es salaam.
Chapisha Maoni