amesema ana deni kubwa la kuwapa furaha
mashabiki wa Msimbazi, ambao kwa miaka minne
mfululizo wamekuwa wakiinamisha vichwa chini
kutokana na timu yao kufanya vibaya Ligi Kuu
Bara.
Akihojiwa na gazeti la Nipashe wakati akijiandaa
kuondoka na timu hiyo kuelekea Morogoro kwa
ajili ya kambi, Kichuya alisema, mapokezi
aliyoyapata kwa mashabiki wa timu hiyo ni kama
amejiandalia deni la kulipa.
"Mashabiki wana imani na mimi, nina kazi ya
kuhakikisha imani yao kwan gu inazaa matunda,"
alisema mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa
Sugar.
Kichuya alisema amejiandaa kukutana na
changamoto mpya kwenye timu hiyo.
"Naamini usajili wangu Simba unatokana na uwezo
wangu, mambo mengine ya namba namuachia
kocha," alisema.
Wiki iliyopita Kichuya alikamilisha usajili wa kuvaa
jezi nyekundu na nyeupe msimu ujao.
Chapisha Maoni