0
Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika mvutano mkubwa na Baraza la Vijana wa
Chadema (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu
Maalum wa chama hicho tawala uliopangwa
kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.
UVCCM wameionya BAVICHA kuhusu mpango
wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma siku
hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa
madai kuwa unakiuka amri halali ya polisi ya
kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya
kisiasa nchini.
Onyo hiyo limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa
UVCCM, Shaka Hamda Shaka ambaye aliwaambia
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam
kuwa watawakabili kwa nguvu zote BAVICHA
endapo wataamua kuendesha siasa zinazolenga
kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na
kutishia maisha.
Alisema umoja huo hautaona shaka kutumia
mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau
miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya.
“Hatutaona muhali kupita njia zilizotumiwa na
wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili kukihami
chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi
na heshima yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu
huyo wa UVCCM.
CCM inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum
Julai 23 mwaka huu ambapo Rais John Magufuli
atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho
kutoka kwa mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.

Chapisha Maoni

 
Top