0
Wanachama na mashabiki wa Yanga, jana jioni walifika nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na
Mawasiliano wa
Simba, Haji Manara na kukabidhi mchango wao
kwa ajili ya matibabu.
Wanayanga hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro na
walimkabidhi Manara kiasi ya Sh 1,055,000 kama
mchango wao.
Wiki iliyopita, Manara aliamka jicho la kushoto halioni. Pia jicho lake la kulia halioni vizuri pia.
Hivyo anatarajiwa kupelekwa India kwa ajili ya matibabu na safari yake huenda ikawa Jumamosi
hii.
Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi mbalimbali ya mitandao ya Wanayanga.
“Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni mdogo sana. Lakini nimkubwa
sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana.
“Nyie sasa mmredusha zile enzi za Yanga na
Simba ambao walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile.
Msiba wa Yanga wanazika Simba, Simba wanazika
Yanga. Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema Manara.

Chapisha Maoni

 
Top