kwamba mshambuliaji wa Italia, Graziano
Pelle amejiunga rasmi na klabu ya
Shandong Luneng ya China. Huu ni
usajili mwingine wa pesa nyingi kwa
mastaa wanaoelekea nchini China baada
ya ule wa Mbrazil Hulk. Pelle ataungana
na mchezaji wa zamani wa Newcastle,
Papiss Cisse klabuni Shandong Luneng.
Hivi ni kwanini Pelle ameamua kujiunga
na Shandong Luneng wakati bado yuko
kwenye ubora wa hali ya juu hasa
ukizingatia kwamba ametoka kufanya
mambo makubwa kwenye michuano ya
Euro iliyomalizika hivi karibuni na
kuisaidia klabu yake ya zamani ya
Southampton kupata nafasi ya kushiriki
michuano ya Ligi ya Europa msimu
ujao? Ni kwa sababu atakuwa akilipwa
euro 350, 000 kwa wiki!
Ni wazi kuwa hii ndiyo sababu kubwa ya
Pelle kuelekea China. Atakuwa akilipwa
mpunga mkubwa mno, ambapo kwa
umri wake wa miaka 30 ni wakati sahihi
mno kwake kwenda kuvuna kiasi
kikubwa kama hicho. Inaweza
kuchukuliwa kama ameenda kujitopeza
katika ramani ya soka, lakini kwa sasa
Pelle atakuwa mchezaji wa 6 duniani
kulipwa mshahara mkubwa zaidi katika
ulimwengu wa soka. Ni Cristiano
Ronaldo, Lionel Messi, Hulk, Neymar na
Zlatan Ibrahimovic pekee kwa sasa ndio
wanamzidi kwa kulipwa vizuri zaidi.
Yaani atakuwa akilipwa euro 50,000 kwa
siku. Muitaliano huyo kwa sasa atakuwa
akipata euro milioni 2.5 kwa mwaka,
pesa nyingi zaidi ya mshambuliaji wa
Bayern Munich na Ujerumani Thomas
Muller. Wanaoongozwa kwa kulipwa
pesa nyingi zaidi kwa mwaka ni: CR7 –
euro milioni 21, Messi – euro milioni 20,
Hulk – euro milioni 20, Neymar – euro
milioni 19, Ibra – euro milioni 16, Pellé
– euro milioni 16, Müller – euro milioni
13.5, Lavezzi – euro milioni 13, Jackson
– 12.5 na Silva – 12.

Chapisha Maoni