Robert Lewandowski amefunga hat-trick ya pili
ndani ya siku nane na kuiwezesha Bayern
Munich kuuanza msimu mpya wa ligi ya
bundesliga kwa kishindo kikubwa baada ya
Ijumaa usiku kuichapa Werder Bremen kwa
jumla ya mabao 6-0 nyumbani Allianz Arena.
Lewandowski ambaye alifunga hat-trick Ijumaa
iliyopita katika ushindi wa Bayern Munich wa
mabao 5-0 dhidi ya Carl Zeiss Jena katika
michuano ya DFB-Pokal amerudia tena hilo jana
ambapo ligi ya Bundesliga ilikuwa inafikisha
msimu wake wa 54 tangu ilipoasisiwa.
Xabi Alonso ndiye aliyeanza kufungua ukurasa
wa mabao baada ya kufunga bao safi dakika ya
9 ya kipindi cha kwanza kabla ya Lewandowski
kuongeza mawili dakika ya 13 na 46 na kufanya
Bayern Munich iende mapumziko ikiwa kifua
mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.
Kipindi cha pili Philip Lahm na Frank Ribery
waliifungia Bayern Munich bao la nne na la tano
dakika za 66 na 73 kabla ya Lewandowski
kuifunga bao la sita kwa mkwaju wa penati
dakika ya 77 baada ya Maximilian Eggestein wa
Weder Bremen kumchezea madhambi Rafinha.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni