Makundi ya ligi ya mabingwa barani yamepangwa
jioni ya leo huko Ufaransa na kushuhudia timu
zikiangukia katika makundi ambayo yataleta
mvuto mkubwa katika hatua hii.
Arsenal wao wako kundi A wakiwa pia na
mabingwa wa Ufaransa PSG, FC Basel ya Uswiss
na Ludogorets ya Bulgaria kundi ambalo wengi
wanazipa nafasi Arsenal na PSG kusonga mbele.
Manchester City wao wamepangwa katika kundi C
wakiwa na Mabingwa wa Spain
Barcelona,Mabingwa wa Scotland Celtic pamoja na
Borussia Mondnglebach ya Ujerumani. Kundi
linaloonekana kuwa gumu kutokana na uimara wa
timu zenyewe lakini hasa uwepo wa Pep Guadiola
katika kikosi cha Man City.
Mabingwa watetezi Real Madrid wamepangwa
kukutana na Borussia Dortmund ya Ujerumani,
Sporting Lisbon ya Ureno na Legia Warsaw ya
Poland.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni