0

MBWANA Samatta amefunga bao moja na kuiwezesha klabu yake ya KRC Genk kutinga
hatua ya makundi ya michuano ya Europa Ligi baada ya usiku huu kuichapa NK Lokomotiva
kwa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa katika uwanja wa Cristal Arena jijini Genk.
Samatta alianza kuifungia KRC Genk dakika ya kwanza ya kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri ya Leon Bailey.
Bao la pili limefungwa na Leon Bailey dakika ya 50 ya kipindi cha pili cha mchezo baada ya
kupokea pasi ya Leandro Trossard.
Matokeo hayo yameifanya KRC Genk iweze kufuzu kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya
mchezo wa awali timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top