Mshambuliaji wa Deportivo La Coruna Lucas Perez
na beki wa Valencia Shkodran Mustafi
wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Arsenal
siku ya Ijumaa kabla ya kujiunga na klabu hiyo.
Gunners wamekubaliana na Valencia kuhusu beki
wa kati Mustafi, 24, ambaye anatarajiwa kutia saini
mkataba wa miaka mitano kwa £35m.
Aidha, wamekubali kutoa euro 20m (£17.1m)
kumnunua mshambuliaji wa Deportivo La Coruna
Perez, 27, aliyefunga mabao 17 kutoka kwa mechi
37 alizocheza msimu uliopita.
Ununuzi huo utapelekea kiasi cha pesa
zilizotumiwa na Arsenal kuwanunua wachezaji
kufika £100m tangu kumalizika kwa msimu
uliopita.
Klabu hiyo imenunua kiungo wa kati Granit Xhaka,
beki Rob Holding, mshambuliaji Takuma Asano na
kiungo wa kati Kelechi Nwakali.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema si
kweli kwamba hataki kutumia pesa kuwanunua
wachezaji.
Hii ni baada ya kushurumiwa na baadhi ya
wachezaji kwamba yeye huwa 'mchoyo sana'
sokoni.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.