0

Klabu ya Manchester City imekamilisha usajili wa
aliyekuwa mlinda mlango wa FC Barcelona, Claudio
Bravo kwa dau la euro mil 18.
Bravo amesaini mkataba wa miaka minne na
atakuwa chaguo la kwanza dhidi ya Joe Hart na
Willy Caballero.
FC Barcelona tayari imekamilisha usajili wa kipa
mwingine kutoka Ajax Jasper Cillessen.
Bravo alijiunga na Barcelona mwaka 2014,
ameiwezesha timu hiyo kutwaa mataji mawili ya
La Liga, taji la ligi ya mabingwa na Fifa Club World
Cup.
Upo uwezekano mkubwa Joe Hart mlinda namba
moja wa Uingereza akatimka ili kulinda namba
yake kwenye kikosi cha kwanza cha Uingereza.
Hart hajamvutia Pep Guardiola kocha mpya wa City
ambaye anapendelea mlinda lango anayeweza
kumudu kucheza kama mlinzi(Sweeper-Keeper).



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top