Manchester United imefanikiwa kushinda mchezo
wake wa tatu kwenye ligi kuu ya Uingereza baada
ya kuichapa kwa taabu Hull City bao 1-0.
United ililazimika kusubiri hadi dakika za majeruhi
kupata bao lake likiwekwa kambani na
mshambuliaji mwenye bahati zaidi klabuni hapo
Marcus Rashford aliyeingia kipindi cha pili.
Hull imeendelea kuwashangaza wengi kutokana na
uimara wake licha klabu hiyo kukabiliwa na
'ukata.'
Kama sio uimara wa safu ya ulinzi ya Hull, Man
United ingeweza kufunga mabao mengi kwani
ilitengeneza nafasi nyingi zaidi, muda mwingi
ilikuwa langoni kwa Hull.
Pogba, Ibrahimovic na Wayne Rooney walikosa
nafasi kadhaa za kufunga.
United imefikisha pointi tisa, kutoka michezo
mitatu. Iko nafasi ya pili nyuma ya Chelsea yenye
pointi tisa pia.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni