0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa ya kutangaza
kumshukuru mlezi wake bwana Mohammed Dewji
kwa kuanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.
Dewji maarufu kama MO tayari ameshaanza kulipia
mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi na
Sekretarieti ya klabu na atafanya hivyo katika
kipindi chote cha mpito kuelekea mabadiliko ya
kimuundo ya klabu.
Mbali ya hayo mfanyabiashara huyo mkubwa
barani Afrika atalipia kodi za nyasi bandia na
gharama nyingine za uendeshaji wa klabu.
Uongozi wa Simba unamshukuru sana MO,
ukizingatia klabu kwa sasa haina mdhamini na
unaamini uwekezaji huo ni chachu ya
kuwarejeshea furaha wanasimba na hatimae
kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya msimu huu na
misimu mingi ijayo.
Mwisho klabu inawaomba washabiki wake
wajitokeze kwa wingi siku ya Jmosi ya Octoba
Mosi pale uwanja wa Taifa,kuishangilia Timu yao
itakapocheza mechi ya ligi dhidi ya Yanga.
Tunaamini mechi hiyo ni mwendelezo wa furaha
kwa wanachama na washabiki wetu kote nchini.
Pia tuwaombe sana kukumbuka kununua tiketi kwa
mawakala wa Selcom waliopo katika maeneo
mbalimbali.
Ikumbukwe tiketi za mechi hii ni za kieletroniki.

Imetolewa na
HAJI S.MANARA.
MKUU WA HABARI SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top