Pambano la mahasimu wa soka nchini Yanga SC
na Simba SC litapigwa siku ya Jumamosi hii katika
uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo
kongwe na kubwa zaidi Tanzania zitavaana katika
mchezo wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara
msimu.
Simba haijapoteza mchezo wowote hadi sasa
kufikia raundi ya 6, wakati mabingwa mara mbili
mfululizo na watetezi wa taji hilo, Yanga ilikubali
kuangusha pointi 3 za kwanza msimu huu
walipochapwa 1-0 na Stand United ya Shinyanga
siku ya Jumapili iliyopita.
Simba wana alama 16 baada ya kucheza game sita
na Yanga wana pointi 10 baada ya kucheza game
tano.
Mwamuzi Martin Saanya kutoka Mkoani Morogoro
atachezesha pambano lake la tatu la mahasimu
hao wa Dar es Salaam huku likitaraji kuwa
pambano lake la Tano linalowakutanisha timu za
mji mmoja ‘Pacha.’
Ni mwamuzi mwenye uwezo wa kutoa maamuzi na
kuyasimamia bila uoga jambo ambalo wakati
mwingine huwashinda waamuzi wengi. Saanya
aliwahi kufungiwa kuchezesha soka kwa muda wa
mwaka mmoja mwaka 2012.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni