0

Celtic imekuwa timu ya kwanza kumuharibia Pep
Guardiola, kocha wa Manchester City rekodi ya
kushinda michezo yote baada ya kuilazimisha City
sare ya mabao 3-3 kwenye mchezo wa ligi ya
mabingwa uliopigwa Jumatano usiku huko
Scortland.
Kabla ya mchezo huo City ilikuwa imecheza
michezo 10 kwenye michuano yote na kushinda
yote, ikiwa ni rekodi ya asilimia 100 kwa
Guardiola.
Mousa Dembele mshambuliaji wa Celtic mwenye
umri wa miaka 20 alikuwa mwiba kwa safu ya
ulinzi ya Manchester City, alipachika mabao mawili
huku Sterling akijifunga bao moja.
Sterling alisawazisha makosa yake baadae kwa
kufungua City bao moja huku Fernadinho na Nolito
nao wakizifumania nyavu pia.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani wa aina yake
kwani timu hizo zilikuwa zikifungana kwa zamu.
FC Barcelona iliyo kundi moja na Celtic, Man City
na Borussia Monchengladbach, iliichapa Borussia
Monchengladbach mabao 2-1 hivyo kukaa kileleni
kwenye msimamo wa kundi F ikiwa na pointi sita.
Katika michezo mingine, Arsenal iliitungua FC
Basel mabao 2-0, Theo Walcott akipachika mabao
yote.
Atletico Madrid imeendelea kuitambia Bayern
Munich baada ya kuilaza bao 1-0 katika mchezo
mwingine wa michuano ya ligi ya mabingwa.
Matokeo yote ya michezo iliyochezwa Jumatano
usiku;




Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top