0

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameiambia BBC
kuwa wachezaji kutoka nchi za Afrika wamekuwa
wenye umuhimu mkubwa katika taaluma yake ya
miaka 20.
Wenga alikuwa akizungumza wakati wa mkutano
wake wa kawaida na waandishi wa habari kabla ya
mechi ambapo pia alitunukiwa kwa kukiongoza
klabu hicho kwa miongo mwili.
Akiwa mwenye uso uliotabasamu, Wenger amesena
kuwa wachezaji kutoa Afrika wana moyo, wenye
ubunifu na nguvu, masuala ambayo ni vigumu
kuyapa kwenye mchezo.
Aliwataja wachezaji akiwemo Nwanko Kanu wa
Nigeria, Kolo Toure wa Ivory Coast na gwiji raia wa
Liberia George Weah, ambaye alikuwa meneja
wake katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa,
kama wachezaji watatu waliokuwa na ushawishi
mkubwa katika taaluma yake.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top